Tuesday, 4 March 2014

UNAAMBIWA LORD EYEZ KAZENGUA TENA, AHUSISHWA NA TUKIO JINGINE LA UWIZI ARUSHA

Mwaka jana ni mwaka ambao memba wa kundi la Weusi ambaye aliwahi kuwepo Nako 2 nako Lord Eyez,kuhusu kuhusishwa na wizi wa mali za msanii mwenzake Ommy Dimpoz,sasa hii imetokea Arusha kwenye wizi unaomhusisha tena Lord Eyez,sikiliza kupitia 87.9 Clouds Fm Arusha.
Bonyeza play kusikiliza.
 
 

MAMBO 10 AMBAYO KILA MSICHANA ALIYE SINGLE ANATAKIWA KUYAFAHAMU. CHEKI HAPA


1. Usiharakishe kutoka nyumbani kwa wazazi wako kwa gia ya kwenda kuolewa.
2. Usimsubiri mwanaume mpaka aje ndio uanze kuishi. Unaweza kuishi maisha timilifu hata ukiwa huna mwanaume.
3.Achana na pombe zimewauwa wenzako wengi kwa kisingizio cha kuondoa stress na wewe unaweza kufa pia.
4. Usiwe mtu wa kuendekeza kuzipokea na kuzijibu namba ngeni za simu hasa nyakati za usiku.. sio njia sahihi ya kupatia mpenzi....
5. Tengeneza mazingira ya kuilinda afya. Jitahidi Kunywa maji mengi na Chakula kwa diet achana na viofa ofa vya bure, vimesha waponza wenzio wengi mpaka sasa.
6. Vaa vizuri na kiheshima. Watu watavutiwa na wewe ulivyo kabla ya kuongea nawe
7.Usitumie sex kama ndio mzani wa mapenzi. Unaweza ukaachika tuu pamoja na penzi lako taamu.
8. Usiolewe na mtu kwa sababu ya fedha; Utabakia kuwa mtumwa wake
9. Jiongezee ubora wako, Tafuta kazi, Usiwe mpuuzi ukaamini mwanaume atatatua matatizo yako yote.
10. Jiheshimu sana kwa kuangalia namna ya uvaaji wa mavazi yako na mwonekano wako mbele ya jamii…. Usitegemee kuvaa kimini ukutane na mwanaume wa suti… wewe utampata wa milegezo na kubana pua tu.
 
 
 

"KATI YA WATU WALIOWAHI KUNIKOSEA SANA NI OSTAZ JUMA" ASEMA NEY WA MITEGO, STORI NZIMA HAPA


Nay wa Mitego: Katika watu waliowahi kunikosea Ostaz Juma amenikosea kupita maelezo, kuliko PNC
Mkasa wa Ostaz Juma na PNC linaweza kutajwa kuwa moja kati ya matukio yaliyozungumzwa zaidi kwa wiki iliyopitwa kupitia mitandao ya kijamii na baadae kuwa topic kwenye radio na television wiki iliyopita.
Ingawa wasanii wengi walilaani kitendo hicho, rapper wa Manzese, Nay wa Mitego yeye aliiambia Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm kuwa kitendo alichokifanya Ostaz Juma kupost picha zinazomuoenesha PNC akimpigia magoti, kwa upande wake amemkosea yeye hata kuliko PNC mwenyewe.
“kumpigia mtu magoti kwa ajili ya kuomba msamaha ni sahihi. Lakini kuna upigiaji wa magoti mwingine ambao baadae unaweza kuonesha picha mbaya kuwa umedhamilia kumdhalilisha. Halafu Ostaz Juma hana nidhamu halafu ni mtu ambaye hajitambui. Vijisenti anavyovipata nadhani ndivyo vinampa jeuri ya kudhalilisha wasanii wenzetu, sio kitu kizuri.

Mimi tangu nilipoona hizo picha nilisema siwezi kumpenda hata siku moja, hata salamu yangu siwezi kumpa. Siwezi kumheshimu hata kidogo. Nitamdharau kuliko kitu chochote, kuliko mtu yeyote aliyewahi kunikosea sana. Ila katika watu ambao waliowahi kunikosea, nafikiri mimi Ostaz Juma amenikosea kupita maelezo. Kuliko alivyomkosea PNC mwenyewe.”
By TimesFm

No comments:

Post a Comment