TUCTA yatishia kutoshiriki Mei Mosi
SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), limetishia kutoshiriki sherehe za Mei Mosi kwa mwaka huu kwa madai kuwa Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kutekeleza madai ya wafanyakazi.
Habari kutoka ndani ya shirikisho hilo zilisema kuwa kwa miaka minne mfululizo Rais Kikwete ameshindwa kutekeleza madai ya wafanyakazi nchini, hivyo hawaoni sababu ya kuendelea kushiriki maadhimisho hayo na kuendelea kutoa madai yale yale kila mwaka.
Vyanzo vyetu vya habari vinasema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutofanyika kwa maandamano ya wafanyakazi kama ilivyo kawaida wakati wa sherehe hizo, lengo likiwa kufikisha ujumbe kimataifa.
No comments:
Post a Comment