Tuesday, 4 March 2014

Madega aomba ‘fear play’ CCM


Madega aomba ‘fear play’ CCMMAKADA watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza kuchuana na mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani katika kuwania nafasi ya ubunge wa Chalinze.

Makada hao ni Imani Madega, Ramadhan Maneno na Omari Kabanga ambao walianza kampeni za kuomba kura ndani ya chama hicho zinazofanyika leo ili kumpata mgombea mmoja atakayepambana na wagombea wa vyama vingine.

Kwa upande wake Madega, ambaye ni Mwanasheria na Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Pwani, aliomba kamati ya uteuzi kufanya uamuzi wa haki.

No comments:

Post a Comment