Tuesday, 4 March 2014

TEC: Hatuna upande Katiba mpya

RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, amesema kuwa kanisa halina msimamo wa pamoja katika suala la muundo wa Serikali ya Muungano unaopendekezwa kwenye Katiba mpya.
Badala yake, Askofu Ngalalekumtwa ameungana na kauli ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, akisema kuwa kiongozi, kundi au muumini ndani ya kanisa anaweza kutoa maoni yake binafsi.
“Mimi ni Rais wa TEC, ni kweli, ninasimamia masuala ya imani na maadili ya kanisa, na hayo ndiyo naweza kutolea tamko, tena baada ya maaskofu kukaa na kukubaliana mambo hayo yanayohusu imani na maadili ya kanisa tu, mengine unayoniuliza ni maoni ya mtu binafsi,” alisema Ngalalekumtwa alipoulizwa msimamo wa kanisa kuhusu aina ya muundo wa serikali ya muungano.

No comments:

Post a Comment