Tuesday, 4 March 2014

Jaji kesi ya Msama, Kisena awaka

JAJI wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, Robert Mziray, amekuja juu kulalamikia taarifa za uamuzi alioutoa katika kesi ya mmiliki wa Kampuni ya UDA, Robert Kisena, mfanyabiashara, Alex Msama na Taasisi ya Kiislamu ya African Kuwait kuripotiwa kwenye vyombo vya habari.

Akizungumza mahakamani hapo jana wakati wa kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa, Jaji Mziray alilitaja gazeti hili kwamba limekuwa likiripoti mwendelezo wa kesi hiyo ambao unaonyesha wazi kwamba upande mmoja haujaridhika na uamuzi alioutoa.

No comments:

Post a Comment