Tuesday, 4 March 2014

Sitta: Sitatishwa

 Sitta: Sitatishwa

 WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye ameteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, amesema kama akichaguliwa kushika wadhifa huo ataiongoza taasisi hiyo kwa haki bila kuogopa mtu wala chama.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, ambapo alisema Bunge Maalumu la Katiba lina changamoto nyingi, ikiwemo misimamo ya kiitikadi ya vyama lakini akasisitiza kuwa atahakikisha analiongoza kwa masilahi ya taifa.

Alisema miongoni mwa sifa yake kubwa ni kutenda haki na kuliendesha Bunge kwa haki, ndiyo maana idadi kubwa ya wajumbe wa Bunge hilo walikuwa wakimpigia ‘debe’ la kuwania nafasi hiyo kabla hata chama hakijapitisha jina lake.

No comments:

Post a Comment