Motisha kwa timu ya taifa Kenya,yalipiwa kutazama kombe la dunia.
Rais Kenyatta amesema yeye pamoja na mke wake waliahidi kuipeleka timu hiyo baada ya kushinda katika moja ya michuano ya ndani ya nchi hiyo.
Kapteni wa timu Jeremy Onyango amesema hiyo ni ndoto ambayo sasa imetimia kwa timu yake.
Kenya ni moja ya nchi zilizofanikiwa duniani kwa upande wa riadha lakini haijawahi kufika mbali na kufanikiwa kuingia katika michuano ya Kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment