Mastaa wa Tanzania walivyowasili uwanja wa Jamuhuri Dodoma leo
Mastaa vijana wa Tanzania kutoka kwenye muziki, movie na sehemu
nyingine wakiwemo mastaa wa soka wameungana pamoja na kutumia ushawishi
wao kuonyesha kwamba wakiamua inawezekana.
Tayari walishaifanya video ya wimbo walioufanya wa miaka 50 ya
Tanzania… leo ndio wanaionyesha kwa mara ya kwanza ambapo Rais Kikwete,
Waziri Mkuu Pinda, Rais wa Znz Dr. Shein, Spika Anne Makinda ni miongoni
mwa wakuu wa serikali watakao ungana nao kwenye uwanja wa Jamuhuri hapa
Dodoma kuanzia saa nane mchana.
No comments:
Post a Comment