Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: mfano familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama ukoo wa akina Mushi,Kimaro, Swai, Massawe, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame. Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha wanatoka Old Moshi na Vunjo. Kavishe,Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe,silayo, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu na Kilema. Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba Foya,na kilawe na kadhalika hutoka Kibosho.Ukoo wa akina Teri wako Mamba Kiria na wachache Sango, Old Moshi na wengine walihamia Maji ya Chai, Mkoa wa Arusha.